Tangu ziara ya Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco kufanyika hapa Tanzania mwaka 2016, kama Taifa la Tanzania tulipata neema kubwa baada ya Rais wetu Dkt. John Joseph Magufuli kuomba msaada wa ujenzi wa msikiti mkubwa zaidi hapa nchini na kujengwa kwa ufadhili wa Taifa la Morocco. Ziara hiyo ilizaa matunda na kupitishwa makubaliano ya ujenzi wa Msikiti huo mkoani Dar es Salaam eneo la wilaya ya Kinondoni, ambapo uongozi wa BAKWATA ndio unasimamia shughuli za ujenzi wake.
Tukumbuke pia hapa nchini, Msikiti wa Gaddafi uliopo makao makuu ya nchi Dodoma kwa kipindi kirefu ndio ulikuwa msikiti mkubwa kuliko mingine yote ndani ya nchi na wa pili ndani ya Afrika Mashariki baada ya mwaka 2008 Kanali Gadaffi kufungua Msikiti mwingine Uganda ambao ndio mkubwa zaidi. Sasa tumepata ujenzi wa Msikiti mkubwa sana na ya tupasa kama watanzania wanufaika tutunze na kuenzi majengo haya ambayo ni nyumba takatifu za ibada kwa makundi ya elfu ya Waislamu.
Muonekano wa Msikiti huo wa Bakwata unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa Sita
wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment