Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam ikishirikiana na Uongozi wa UVCCM Tawi la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Uongozi wa UVCCM Tawi la Chuo cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki unapenda kutangaza na kuwakaribisha vijana na wanaharakati katika Mkutano utakaofanyika Ukumbi wa Mwinyi uliopo ndani ya kituo cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kinondoni Biafra tarehe 05/07/2020, saa tatu asubuhi.
Mkutano huu utahusisha agenda kuu mbili, moja ni kumpongeza Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa juhudi, weledi na udalifu wa kazi nzuri aliyofanya ndani ya miaka mitano ya awamu ya kwanza katika serikali ya awamu ya tano anayoingoza. Pili ni mada itakayo zungumzia mafanikio ya serikali katika sekta ya afya hasa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya korona, na kudadavua utekelezaji wa sera ya maendeleo ya vijana.
Mkutano utausisha vijana wa ngazi mbalimbali, kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu, taasisi za jamii na kiraia, makundi ya vijana wa kutoka kwenye shughuli rasmi na wengine wenye mapenzi na uzalendo mwema na taifa la Tanzania. Kwa vijana wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni vyema kuzingatia uvaaji mavazi rasmi ya uanachama na kutakuwa na uuzaji wa mavazi ya chama na vitu vingine vya CCM kwa wale watakaohitaji ili kuwa nadhifu hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Mgeni rasmi wa Mkutano huu atakuwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana Chama Cha mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ndg. Galila Wabanhu akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa wilaya na kata za Kinondoni pamoja na viongozi wa matawi ya vyuo hivi viwili akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Ndg. Rogers Mgonja, Katibu Ndg. Given George, Katibu Hamasa Ndg. Issa J. Issa, Wajumbe Ndg. Mary Hamisi na Ndg. Benson Kaile, kutoka Chuo cha Hubert Kairuki Mwenyekiti wake, Katibu Ndg. Luciana Mduma, Katibu Hamasa Ndg. Gladness Beda Shayo na Mjumbe Ndg. Rose Shondi.
“VIJANA IMARA, UZALENDO IMARA”
No comments:
Post a Comment