Kubwa kuliko ni serikali kuanzisha miradi mipya ya miundombinu itakayowezesha utendaji wa shughuli za kiuchumi kuwa mkubwa na wa kasi zaidi hasa katika kuunganisha masoko ya Afrika Mashariki na Kati pamoja na nchi wanachama za kusini (SADC). Ujenzi wa reli ya kati ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) ni reli itakayotumia nishati ya umeme na kuwa na ufanisi wa safari za haraka zaidi kutoka pwani ya Tanzania Dar es Salaam na mkoa wa Pwani kupita katikakati ya nchi yaani Morogoro, Dodoma, Tabora, Singida, Shinyanga na Mwanza. Baadae ujenzi unategemea hadi taifa la Rwanda. Serikali imetoa zaidi ya Trilioni 7 za Kitanzania kufadhili mradi huu baada ya ufadhili na mikopo kutoka nje ya nchi kususua.
B
Thursday, July 9, 2020
MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE TANZANIA
Tanzani kuwa na mipango ya kuingia kwenye uchumi wa kati kitaifa na kimataifa ni jambo ambalo limefanikiwa mwaka 2020 sambamba na miradi mikubwa inayobuniwa na kutekelezwa na serikali iliyopo madarakani tangu mwaka 2015. Tanzania ina tawaliwa na Chama kikongwe cha siasa Afrika na ulimwenguni kwa ujumla, Chama cha Mapinduzi. Katika ilani ya uchaguzi wa mwaka 2015 kupitia mgombea wake Dkt. John Joseph Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Tanzania, chama cha CCM kilijinadi kufanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya uchumi hasa kufufua sekta viwanda, sekta ya usafirishaji na uchukuzi kama kufufua shirika la ndege la taifa, kuimarisha na kuboresha safu ya nishati na rasilimali za taifa zilizohujumiwa vibaya katika miongo ya uongozi wa nyuma kutokana na viongozi wasio waadilifu, mfano madini pamoja na ujenzi wa bwala la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment