B

B

Saturday, August 13, 2016

MSANII WA BONGO FLEVA DIAMOND PLATNUMZ ATHIBITISHA KUWA NA UTAJIRI WA TAKRIBANI USD MILLION 4 (TZS 8.8 BILIONI) NETWORH

Afrika Mashariki na Kati hutoweza kuonngelea sanaa na mziki kwa sasa bila kumtaja Msanii wa Kitanzania Diamond Platnumz alias Nasib Abdul. Msanii huyu anayefanya kazi zake kwa vionjo vya Bongo Fleva na Afro Pop huku akijizolea umaarufu mkubwa kitaifa na kimataifa kwa kufanya matamasha mengi na kunyakua tuzo nyingi tofautii tofauti. Pia Msanii huyu ni Balozi wa Makampuni mbalimbali makubwa nje na ndani ya Tanzania kama DSTV multi choice, Red Gold, Vodacom, Coca Cola, Uber na nyinginezo. Kwa taarifa ambazo hazijadhibitika kiundani zinasema kuwa Diamond Platnumz anadau la kuanzia Tshs milioni 7.9 hadi Tshs milioni 8 kwa matamasha ya ndani ya nchi na kujiweka katika viwango vizuri kimataifa kwa zaidi ya dau la Tshs milioni 51.6 na kuendelea.
Mwanamziki Diamond ambaye anashikilia rekodi kubwa ya kushinda Tuzo nyingi pia anamejizolea na kuendelea kujizolea utajiri zaidi kupitia milio ya simu yenye nyimbo zake na ndio msanii pekee ambaye hupendelewa sana kimachaguo ya miito ya simu kitaifa. Pia nyimbo zake hushikilia rekodi nzuri za upakuaji kwenye mitandao mbalimbali ndani na nje ya Taifa la Tanzania.
Pia msanii huyu ana vitega uchumi vingi kama Real estates properties zikiwemo apartments, viwanja na biashara mbalimbali jiji Dar es Salaam. Kwasasa amewekeza pia katika lebo yake mpya ijulikanayo kama Wasafi Classic Baby (WCB) nyeneye wasanii maarufu kama Rich Mavoko na Queen Darling na wengine chipukizi kama Harmonize na Rayvan. Hadi sasa Msanii Diamond Platnumz amefikisha nyimbo zaidi ya 150 kama yeye binafsi na kiushirikishaji ndani na nje ya Tanzania.
     

No comments:

Post a Comment