B

B

Friday, December 20, 2013

P SQUIRE WATOA MISAADA KWA WATOTO WENYE UGONJWA WA AKILI

Wasanii mapacha Peter Okoye na Paul Okoye wanaotamba kwenye fani ya muziki wa Africa na dunia kwa ujumla wamefanya jambo la ukarimu kwa watoto wenye matatizo ya akili kwenye kituo kilichopo hapa jijini. Tukio hili lilifanyika baada ya wasanii hawa kumaliza shoo yao waliyokuja kuifanya Tanzania na kuweza kumaliza kiu ya watanzania walio wengi walioweza kuwashuhudia wasanii hawa wanaotamba na kibao chao kikali kiitwacho Personally kwa shoo kali iliyofanyika viwanja vya Leaders tarehe 23 october 2013. Uongozi wa kituo uliwashukuru kwa dhati wasanii hao kwa moyo mkunjufu kwa vijana wao wanaowalea katika mazingira magumu. Wasanii hawa wameshaondoka nchini kwa ajili ya shughuli zao nyingine za kimuziki wakizunguka nchi mbalimbali kote duniani kupiga concerts kadhaa kabla hawajaachia album yao mpya inayokuja hivi karibuni.Hii ni mara ya pili P square kuja nchini kufanya shoo inayoandaliwa na IPP Media chini ya EATV. Mr.Paul Okoye november mwaka huu amebahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa na mpenzi wake walipata mtoto wa kiume...



                  Report by;Benson kaile

No comments:

Post a Comment