JE WAJUA KUWA RAPPER LIL WAYNE NI SHABIKI WA SOKA
MSANII WA HIP HOP LIL WAYNE NI SHABIKI WA CHELSEA
Rapper wa Hip Hop ajulikanae kama DYWANE CARTER Jr. kwa jina la kisanii akitambulika kama Lil Wayne,ameonyesha hali ya kuthamini michezo ukiachilia nyuma na kazi ya mziki anayoifanya.Mwanamziki huyu wa Hip Hop ambaye ni shabiki mkubwa wa michezo ya kikapu nchini kwao marekani hasa akishabikia team ya Hornets iliyopo kwenye makazi aliyokulia huko New Orleans.Ila imesikika akishabikia Miami Heats huku Kobe Bryant akiwa mchezaji bora kwake anayekiputa LA Lakers.Msanii huyu pia ameweonyesha pia ni mtu ambaye ni shabiki wa mpira wa miguu akiwa mstari wa mbele kwenye ligi kuu ya Uingereza akiifagilia kwa bashasha club ya CHELSEA FC yenye makazi yake Stamford Bridge.Amekuwa mara kwa mara akitweet kuhusu Club hii na kuvaa nguo mbalimbali kwenye mitoko yake ikiwa na nembo ya Club ya Chelsea na pia kuisifia mara kwa mara.
Report by;Benson kaile
No comments:
Post a Comment