B

B

Saturday, December 21, 2013

BREAKING NEWS!!! MOTO WAWAKA BUNGENI-KAGASHEKI AJIONDOA, NCHIMBI NAODHA NA MATHAYO WAENGULIWA

Waziri wa maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akisisitiza jambo juu ya mswada wa leo Bungeni Dododma.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesisitiza kuwa hakuna shaka kwani waliohusika wote na taasisi zao zichunguzwe kiundani mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe. Kulinda rasilimali za Taifa amenena kuwa ni la muhimu. Pia alisema aliongea na waziri mmoja mmoja nakuona ni busara ushauri wa wabunge utekelezwe. Na kuwa ameongea na Rais na kukubali utenguzi wa mawaziri hao.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Bw. David Mathayo akijitetea baada ya kuona ameonewa juu ya shutuma zilizopo kwenye mjadala uliokuwa Bungeni leo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki amjiuzulu wadhifa wake baada ya mjadala mkali uluiokuwa ukiendelea leo Bungeni Dodoma. Hiii imetokana na operation Tokomeza inayoendelea nchini ikiwa nikupambana na kuondoa ujangili uliokidhiri nchini. Tangu kuanzishwa kwa operation hiyo, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wabunge, wanaharakati na wananchi dhidi ya askari waliokuwa wakiiendesha operation hii, dhidi ya watu kujeruhiwa, kuchomewa makazi moto, mifugo kuibiwa, kupigwa na uporaji. Operasheni hiyo ilikuwa ikiendeshwa pia na askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), polisi, usalama wa Taifa na Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA). Operesheni hiyo ilizuiwa baada ya suala hilo kutinga Bungeni na watunga sheria hao kuweka kando tofauti zao kiitikadi na kuungana wakitaka Waziri Mkuu , Mizengo Pinda, Waziri wa maliasili na Utalii na Waziri wa mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, David Mathayo wawajibike..

No comments:

Post a Comment