B

B

Friday, December 16, 2016

HATIMAYE MWANZILISHI MWENZA WA JAMII FORUM BW. MAXENCE MELO AMEACHIWA HURU KWA DHAMANA. #FREEMASSMEDIA

 



Mwanzilishi mwenza wa mtandao wa kijamii wa maarufu ujulikanao kama Jamii Forum, Bw. Maxence Melo Mubyazi alifikishiwa kwenye vyombo vya usalama tarehe 14/12/2016 `kwa kutaa kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao wa Jamii forum, kitu ambacho amekiwekea msimamo wakutofanya alivyoamriwa ikiwa kama uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi. Maxence alitiwa chini ya ulinzi zaidi ya masaa ishirini na nne bila kufikishwa mahakamani huku ikiwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977,Ibara ya 15 inayotoa haki kwa kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru. 
Maxence anakamatwa kukiwa na kesi ya kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu tarehe 20 Februari. 
Maxence amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam na kushtakiwa kwa makosa matatu likiwemo lakuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini kinyume na sheria. Makosa mengine mawili aliyoshtakiwa nayo ni kuzuia uchunguzi wa Jeshi la polisi, la tatu limemfanya Max kutoweza kupewa dhamana kwa kutosajili tovuti yao kwa kikoa cha (.com) badala ya (.co.tz) jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume na sheria. Max amepelekwa gereza la keko mpaka Jumatatu. #FREEMAXENCEMELO2016 #FREEMAXENCEMELO  #JAMIIFORUMS

No comments:

Post a Comment